Mwanafunzi wa miaka 13 Aolewa Tabora, Mama Mzazi ahusika Kumuozesha

Mwanafunzi wa shule ya Msingi Rufita iliyoko mkoani Tabora mwenye umri wa miaka 13 ameozeshwa kinyemela na mama yake Mzazi na kukatishwa masomo

Mwanafunzi huyo anayeishi na mwanaume anayejulikana kwa jina la Bakari Abdul Kwa muda wa miezi mitatu sasa huku mzazi wa mwanafunzi huyo akidai hajui mwanaye aliko

Walimu wa mwanafunzi huyo ambaye jina lake limehifadhiwa wamesema alikuwa mtoro na kwamba mzazi wake hakuwa akitoa ushirikiano kwao


Afisa mtendaji wa kata ya Mbugani ilipo shule hiyo Imakulata Gembe amesema wamechukua hatua ikiwemo kuwakamata wazazi wa mwanafunzi huyo ili iwe fundisho kwa wengine


Hivi karibuni Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri aliagiza mkuu wa wilaya kuwashughulikia wale wote wanaowakataza watoto wa kike wasisome na kwamba wawe wakali hata kwa wazazi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo