Mahafali ya 22 Mwakavuta Sekondari Makete Yanoga Balaa

 wahitimu hao


Wahitimu wa Kidato cha Nne wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kutii mamlaka zilizopo katika maeneo yao watakayokwenda baada ya kuhitimu masomo yao

Hayo yamesema jana na Mgeni Rasmi Mh Sarah Shembekeza katika mahafali ya 22 ya kidato cha Nne katika shule ya Sekondari Mwakavuta, ambapo amewasisitiza wanafunzi hao kuwa mbali na kuhakikisha wanafanya vema katika mtihani wa kuhitimu kidato cha nne lakini pia watambue kuna mamlaka watakazokutana nazo baada ya kuhitimu na wanatakiwa kuziheshimu

Pia amewaonya suala la kuvaa mavazi isivyokubalika


Amewataka wawapo vijijini kujiepusha na makundi mabaya yatakayoweza kuwashawishi kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya na utumiaji wa pombe


Akijibu baadhi ya changamoto Mh Shembekeza amesema atapigania kuhakikisha kero ya maji inayoikabili shule hiyo kutokana na ongezeko la watumiaji wa huduma hiyo linamalizika kutokana na mipango ambayo imewekwa na halmashauri ya wilaya ya Makete


Katika mahafali hayo Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Lukas Mkakatu akazungumzia pia baadhi ya mafanikio ya shule hiyo



Nao wahitimu hao wamezungumzia matarajio yao ikiwemo pia kufanya vizuri katika mtihani wao wa kuhitimu kidato cha nne unaotarajiwa kuanza Novemba Mosi Mwaka huu


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo