Kuhusu Ajali ya Ndege iliyotokea Arusha

Watu watano wamenusurika kifo baada ya ndege waliokuwa  wanasafiria kutoka katika uwanja mdogo wa Arusha kupata hitilafu  kwenye injini yake muda mfupi baada ya kuruka.

Kaimu meneja wa uwanja wa ndege wa Arusha Bw, Bashiru Juma  amesema ajali hiyo imetokea saa sita na dakika hamsini na tano ikiwa  ni dakika tano tu baada ya kuruka ikiwa na abiria wanne na rubani  mmoja ikiwa inatoka kwenye uwanja huo kwenda kwenye uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Kimanjaro.

Kwa mujibu wa Bw Bashiru ajali hiyo ya ndege aina ya Caravan 5h  Zeb ya kampuni ya Coastal Air haikuleta madhara na abiria wote pamoja na rubani wametoka salama na pia hakuna uharibifu wowote  unaoonekana kwa macho kwenye ndege hoyo na kwamba taratibu vyombo  vinavyohusika na masuala ya anga kuchunguza tukio hilo  zinaendelea.

Kwa upande mtendaji wa kampuni ya hiyo ya Caoastal Air nchini  Capten Dmond Julian amesema abiria walikuwa wanne wawili raia wa  ujerumani na wawili raia wa italia na walikuwa walikuwa wanakwenda  Zanzibar.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo