Jela Maisha baada ya Kumlawiti Mwanaume aliyemfumania na Mkewe Gesti

Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemhukumu kifungo cha maisha jela, Erick Kasila (39) baada ya kupatikana na hatia katika mashtaka matatu likiwamo la kumlawiti mwanamume kwa madai kuwa alimfumania gesti na akiwa na mke wake.

Kasila anadaiwa kumlawiti Idd Kambi katika nyumba ya kulala Wageni ya Maembe, Yombo Kiwalani, Wilaya ya Ilala na kumpiga picha za utupu na kutisha kuzitumia katika mitandao ya kijamii na kumnyang’anya nguo alizovaa, fedha, laptop na viatu.

Mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Juma Richard (31) alihukumiwa kifungo cha miaka 14 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlazimisha mlalamikaji kumnyonya uume wake na kumtaka kusaini karatasi ya ahadi ya Sh1 milioni ili asisambaze picha walizompiga wakati wakimlawiti, ambazo hata hivyo, walizisambaza katika mitandao ya kijamii.

Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Said Mkasiwa alisema ameridhishwa na ushahidi wa mashahidi watano dhidi ya washtakiwa na vielelezo vya picha zinazoonyesha mlalamikaji alikuwa analawitiwa, nyingine zikionyesha mshtakiwa akimlazimisha mlalamikaji amnyonye sehemu zake za siri.

Akipitia baadhi ya ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, Hakimu Mkasiwa alisema kulawitiwa kwa mwanamume huyo ni baada ya kukutwa na Sanifa Bakari ambaye ni mke wa Kasila.

Kabla ya hukumu hiyo, upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Silvia Mitanto uliiomba Mahakama kutoa adhabu kali dhidi ya washtakiwa hao kwa kitendo walichokifanya ambacho kimemuathiri mlalamikaji kisaikolojia.

Washtakiwa walipopewa nafasi ya kujitetea kwa nini wasipewe adhabu kali, walishindwa na badala yake waliomba nakala ya hukumu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo