Halmashauri yapigwa Faini ya Milioni 12, Kisa Takataka zimewashinda

Baraza la Taifa na uhifadhi na usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC) limeitoza faini ya shilingi Milioni 12, Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, kutokana na kutoweka mundombinu ya kukusanya taka ngumu, kuziacha eneo la shughuli za watu kwa mda wa zaidi ya mwezi mmoja, hali ambayo inaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa. 

Hatua hiyo ya kuitoza faini manispaa ya Tabora imetokana na ziara ya kushitukiza Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga Jackson Mpina, aliyoifanya katika siko kuu la mjini Tabora, na kubaini taka ngumu zamda mlefu, ambapo amepokea malalamiko ya wafanya biashara wakidai kuwa,uongozi wa manispaa umewatelekeza. 

Akizungumza na wafanyabiashara hao mara baada ya kumuhoji mkurugenzi wa manispaa hiyo,Bw, Bosco Ndunguru, ambaye amekiri kuwepo na changamoto ya ukusanyaji taka,Mhe,Luhaga Mpina, amesema, Serikali haitawavumilia watendaji ambao hawatimizi wajibu wao kwa wananchi.

Akitoa adhabu hiyo ambayo imedaiwa kuwa ni ya kwanza NEMC kuiwajibisha halmashauri, afisa  Mazingira Mwandamizi, Bw. Benjamini Doto amesema kuwa, baraza limefikia maamuzi hayo baada ya kujiridhisha juu ya uzembe wa uzoaji taka ngumu wakati ni wajibu wa Halmashauri kuweka mikakati ya kufanya usafi maeneo ya biashara.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo