Katika kuadhimisha miaka 17 ya kifo cha baba wa taifa
Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, wanafunzi wilayani Makete Mkoani Njombe
wametakiwa kusoma kwa bidii kwa kuwa taifa linawategemea ikiwemo kuja kushika
nyadhifa mbalimbali baada ya kuhitimu masomo yao
Kauli hiyo imetolewa jana na Mgeni Rasmi katika
maadhimisho ya miaka 17 ya kifo cha Baba wa taifa mwalimu Julius Nyerere ambaye
pia ni Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kessi yaliyoadhimishwa kiwilaya
katika shule ya Sekondari Lupalilo
Aidha Mkuu huyo ametoa Onyo kali kwa walimu wote
wanaojihusisha kimapenzi na wanafunzi na kusema sheria zipo wazi kwa yeyote
atakayebainika atachukuliwa hatua, huku akiwataka wanaofanya hivyo kama wapo
kuacha vitendo hivyo mara moja
Naye diwani wa kata ya Tandala Mh Egnatio Mtawa ambaye
pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete akishukuru kwa hotuba ya
mgeni rasmi amesisitiza maagizo hayo wahusika wayafanyie kazi ili kuepusha
madahara yatakayoweza kujitokeza endapo maagizo hayo yatapuuzwa
Awali katika maadhimisho hayo pamoja na mambo mengine
wanafunzi wa shule ya sekondari Lupalilo wamepatiwa elimu ya Virusi vya Ukimwi
na UKIMWI kazi iliyofanywa na Mratibu wa Ukimwi sekta zote Wilaya ya Makete Bi
Ester Lamosai ambapo pamoja na mambo mengine amemueleza mgeni rasmi jinsi
ambavyo shule nyingi hazipo salama kwa sasa