Na Faustine Fabian, Mwananchi
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Simiyu imewaachia kwa dhamana Naibu Katibu Mkuu wa Chadema- Zanzibar, Salum Mwalimu na wenzake Oscar kaijage na Renatus Nzemo
Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo John Mkwabi alisema kuwa kutokana hoja zilizowasilishwa na upande wa mashtaka za kuzuia dhamana kutokuwa na tija hivyo kutupiliwa mbali.
Mkwabi alisema washtakiwa hao wamedhaminiwa kwa masharti ya hati ya dhamana ya Sh 20 milioni na kuwa na wadhamini wawili.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 4, 2016 watakapoletwa tena mahakamani.
