Majibu ya Serikali Bungeni kwa swali la Mbunge Norman Sigalla kuhusu Shamba la Kitulo

Serikali imesema inakusudia kuliboresha shamba la mifugo la Kitulo Lililopo wilayani Makete mkoani Njombe ili liwe na manufaa zaidi kwa wakazi wa wilaya hiyo na wilaya nyingine za mkoa wa Njombe

Kauli hiyo ya serikali imetolewa leo Bungeni Dodoma na Naibu waziri wa Kilimo mifugo na Uvuvi Willium Ole Nasha wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Makete Prof Norman Sigalla lililotaka kufahamu mipango ya serikali ya kuhakikisha wanamakete wananufaika na uwepo wa shamba hilo

Akiuliza swali la nyongeza kwa niaba ya Prof Norman, Mbunge wa Makambako Deo Sanga ameitaka serikali kueleza manufaa ya shamba hilo kwa mkoa mzima wa Njombe Ikiwemo wananchi kukopeshwa ng'ombe katika shamba hilo la Kitulo na naibu waziri akatoa ufafanuzi wa suala hilo kuwa serikali ipo tayari kushirikiana na halmashauri hizo ili suala hilo lifanikiwe


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo