Kutoka Ikulu: Rais Magufuli Atasafiri kwenda Nje ya Nchi kwa siku tatu kuanzia Kesho


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kesho tarehe 12 Septemba, 2016 anatarajiwa kuwasili Mjini Lusaka nchini Zambia kwa ziara ya siku tatu ambapo pamoja na mambo mengine atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu zitakazofanyika keshokutwa tarehe 13 Septemba, 2016 katika Jiji la Lusaka.

Rais Magufuli anafanya ziara hii ya kwanza nchini Zambia akiwa pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa,Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Kamati hiyo inajulikana kwa jina la SADC-Troika.

Dkt. Magufuli alipokea kijiti cha Uenyekiti wa SADC-Troika kutoka kwa Rais wa nne Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi katika Mkutano wa 36 wa SADC uliofanyika katika Jiji la Mbabane nchini Swaziland tarehe 01 Septemba, 2016.

Katika Ziara hii Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na Viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika watakaohudhuria sherehe hizo zitakazofanyika katika Uwanja wa Mashujaa Jijini Lusaka.
 
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Lusaka

11 Septemba, 2016


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo