Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),kimelitaka jeshi la polisi kuwaachia au kuwapeleka mahakamani watu 10 wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa chama hicho.
Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu amewaambia wanahabari leo kuwa watu hao walikamatwa katika mikoa mbalimbali ukiwamo wa Songwe kwa kosa la kuandika na kusambaza maneno yasiyomfaa Rais John Magufuli.
Lissu amesema watu wapo mahabusu za Polisi Kanda Maalumu na Osterbay takriban wiki zaidi ya mbili jambo ambao ni kinyume cha sheria za nchi na kwamba wanapewa mateso.
"Nimekwenda kuonana nao na wamenieleza madhara wanayoyapata kutoka kwa polisi,"amesema Lissu.