Amuua mwenzie wakati wakigombania Sola

Mkazi wa Kijiji cha Nkome, wilayani hapa amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kumuua Neema Daniel (24) kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali wakati wakigombania sola.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Issack Msengi amesema umeme huo wa sola ulikuwa umeazimwa na Daniel, hivyo mtuhumiwa alipokuwa anadai kurudishiwa ndiyo kukatokea ugomvi.

Msengi amesema mtuhumiwa alimchoma Daniel na kitu chenye ncha kali kifuani na kufariki dunia papo hapo.

Kamanda huyo amesema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani baada ya kuhojiwa na polisi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo