Tukio la mauaji ya Askari
Polisi wanne katika shambulizi lililofanywa na majambazi katika Bank ya
CRDB Mbande, Dar es salaam Ni Moja ya headline zilizochukua nafasi
kuanzia usiku wa August 23 2016.
Leo August 25 2016 baadhi viongozi wa Serikali akiwemo Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda wameungana na watanzania wengine kuaga miili hiyo ya marehemu.
Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba
aliposimama kuongea na waomboleza pia ametaka wale wote
walioshiriki kuandika mambo ya kufurahishwa katika tukio hilo wakamatwe.
