WALIMU
wakuu wa shule 68 wa shule za Msingi wanatakiwa kuvuliwa na
kunyang'anywa vyeo vyao kwa kosa la udananyifu wa takwimu za wanafunzi
hewa tangu elimu itangazwe kuwa bure.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Salum Hapi wakati
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Amesema
kuwa walimu wakuu hao wametakiwa kuvuliwa vyeo vyao na kuwapa walimu
wengine kwa kosa la kutoa takwimu za wanafunzi hewa 3462 wa shule za
msingi 68 za Wilaya ya Kinondoni. Pia hatua kali za Kisheria
zitachukuliwa kwa dhidi ya walimu wakuu wa shule hizo.
Pia
Hapi amemwomba Katibu Tawala wa Mkoa kuwavua vyeo wakuu wa shule 22 wa
shule za Sekondari 22 za Manispaa ya Kinondoni na Ubungo kwa kosa la
kutoa takwimu za uongo na kuweka wanafunzi hewa.
Wakuu
wa shule za Msingi hao wamekuwa na wanafunzi hewa 2534 kutoka shule 22
za Sekondari za Manispaa ya Kinondoni na Manispaa ya Ubungo.
Wakuu
wa shule hizo wameisababishia Serikali kupoteza zaidi ya shilingi
milioni 60 kwa kupeleka fedha za kuwahudumia wanafunzi wanaosoma katika
shule hizo.