Waifukua maiti ya mhubiri na kumzika kondoo

Wakaazi wa kijiji cha Katituni katika kaunti ya machakos walishangazwa na tukio la familia moja iliyoifukua maiti ya mhubiri mmoja na kumzika kondoo.

Wakazi wakijiji cha Katituni katika kaunti ya machakos walishangazwa na tukio la familia moja la kufukua mwili wa jamaa aliyekuwa amezikwa siku tatu zilizopita.

Jonathan Mutisya Mwania ambaye alikuwa mchungaji wa kanisa la African Brotherhood alikuwa ameaga dunia na mwili wake kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia wafu katika kaunti hiyo.

Inasemekana kwamba mwili wa mhubiri Mutsyia uliwachanganya watu wa familia huku wakiuchukua mwili wa John Ndambuki na kuuizika.

Siku tatu baadae, familia hiyo ilijulishwa kwamba maiti iliyozikwa haikuwa yao, jambo lililowapelekea wazee wa jamii ya Wakamba kuamrishwa kufukuliwa kwa mwili huo.

Baada ya kufukuliwa, mwili huo wa Ndambuki ulirejeshwa katika chumba cha kuhifadhi wafu katika kaunti hiyo, kama njia ya kuzuia mikosi, kulingana na tamaduni za familia hiyo.

Baada ya kuufukua mwili huyo walimuua kondo na kumzika katika kaburi hilo.

Mwili wake Ndambuki tayari umezikwa katika kijiji cha Muisuni, kaunti ya Mwala huku wa mchungaji Mutisya ukisemekana kuwa katika chumba cha kuhifadhi wafu katika kaunti ya Machakos.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo