Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepokea Hati ya kifo cha mshitakiwa wa Saba Katika Kesi inayowakabili wataalam wa teknolojia na mawasiliano wanaotuhumiwa kusambaza matokeo ya uchaguzi Mkuu wa 2015 Kabla ya kuthibitishwa na tume ya Uchaguzi (NEC).

Katika shauri hilo mshitakiwa namba saba ni Jose Nim (51) raia wa Paris Ufaransa wengine ni Mashinda Mtei (49) mkazi wa Tengeru Arusha, Julius Mwita (40) mkazi wa Magomeni Dar es Salaam, Frederick Fussi (25) IT, mkazi wa Mbezi Dar es Salaam, Julius Matei (45) raia wa Kenya, Meshack Mlawa (25) mchungaji na ni mkazi wa Keko, Anisa Rulanyan (41) Mhandisi, mkazi wa Kawe.

Hakimu Respesious Mwijage amesema kuwa pamoja na kuwa imeletwa hati ya kifo mahakama itafanya uchunguzi na kujiridhisha juu ya taarifa za hati hiyo.

Salim Msemo wakili wa serikali ameomba Tahere nyengine ya kutajwa kwa kesi hiyo.
Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 15 Agosti mwaka huu.

Katika kesi hiyo namba 267 ya mwaka 2015 yenye mashtaka matatu pamoja na kutoa taarifa za uongo kwenye mitandao wakati wakijua hazijathibitishwa.

Shitaka la pili linamkabili Julius Matei, Nimi, ambapo wanashtakiwa kuwa Oktoba 26 2015 , wakiwa katika hoteli ya King iliyopo Kinondoni , Dar es Salaam wakiwa na hati za kusafirilia zenye namba A1532119, 930879 na M 27687807 walijiingiza katika ajira ya kukusanya na kusambaza matokeo ya urais ya uchaguzi wa mwaka huu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema ) bila kibali.

Shtaka la tatu linamkabili Julius Matei pekee yake ambaye ni raia wa Kenya mwenye hati ya kusafirilia namba A1532119 akiwa ndani ya jiji la Dar es Salaam alijihusisha na biashara katika Saccos ya Wanama bila kibali.