Mtoto mmoja afariki dunia na wanafunzi wawili wanusurika kufa

WANAFUNZI wawili wanaosoma katika shule ya msingi mgomba Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani wamenusurika kupoteza maisha baada ya nyumba waliyokuwa wamelala kuteketea na moto na kusababisha kifo cha mtoto  mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi tisa anayejulikana kwa jina la Nasma Rajabu.

Moto huo ambao  unasemekana ulitokana  na kuacha  kibatali kikiwa kinawaka  uliweza kuteketeza vitu vyote ambavyo vilikuwemo ndani ya nyumba hiyo pamoja na mtoto mdogo ambaye alishindwa kuokolewa  kutokana moto huo kuwa mkubwa na  kufariki dunia.

 Wakizungumza na kwa masikitiko makubwa katika kijiji hicho akiwemo Abdalah Kitumbi na Nasra Kitumbi wamesema kwamba wakati wamelala majira ya saa  4 usiku walianza kuona moto unawake ndipo walipoamua kukimbia na kutoka nje ya nyumba  kwa ajili ya kuomba msaada.

“Sisi tulikuwa chumbani tumelala mara tukaanza kuona moshi mkubwa, ikabidi tuamke na kukimbia nje kwa ajili ya kuomba msaada lakini kumbe mwenzetu mmoja kwa bahati mbaya alikuwa amebakia ndani na hivyo hakapoteza masiha kutokana na kuungua na moto,”alisema watoto hao.


Aidha walisema kwamba pindi walipokuwa nje moto ulikuwa tayari umeshaanza kusambaa katika mabati hivyo wakashindwa kuuzima na kwamba vifaa vyao vyote vya shule yakiwemo madaftari, pamoja na nguzo zote zimeteketea kwa moto hivyo wameomba wapatiwe msaada kutoka kwa wadau mbali mbali wa maendeleo.


Kwa upande wake  Mbunge wa jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa baada ya kutokea kwa  janga hilo la moto ilimlazimu kusitisha ziara yake ya kikazi na kuwenda  katika eneo la tukio kwa ajili ya kutoa pole na salamu za rambi rambi kwa familia ambapo aliahidi kuwasaidia ujenzi wa nyumba hiyo pamoja na wanafunzi hao kuwanunulia vifaa vyote vya shule vilivyoteketea.


Mchengerwa alisema kwamba janga hilo la moto ni kubwa sana hivyo atahakikisha kwamba anaisaidia familia hiyo kwa hali na mali katika ujenzi wa nyumba iliyoungua sambamba na kuwapatia vifaa vyote wanafunzi hao ili waweze kuendelea na masomo yao kama kamawaida na kuweza kupata sehemu nyingine ya kujihifadhi.


“Mimi kama mbunge wa Jimbo hii la rufiji kwa tukio hili limenigusa sana na nitahakikisha kwamba wanafunzi hawa wanaendelea na masomo yao kama kawaida hivyo nitawanunulia vitu vyote na mahitaji ambayo wanastahii pamoja na kuona ni namna gani tunafanya ujenzi wa nyumba ambayo imeungua ili waweze kupata sehemu ya kujihifadhi, kwani jukumu letu ni kuwasaidia wananchi,”alisema Mchengerwa.


Naye Babu yake na marehemu  Chriss Kitumbi  amebainisha kwamba moto wakati unawake wao pamoja na mke wake  walikuwa wamelala  katika nyumba nyingine ambayo ipo jirani na kwamba walipotoka nje walikuwa moto tayari umeshashika mpaka kwenye bati hivyo kushindwa kuuzima kwa wakati.


Tulia Ngwele yeye ni mama mzazi kwa watoto wawili walionusurika kifo katikia tukio hilo la kuteketea kwa nyumba nzima yeye anaelezea jinsi hali ilivyokuwa baada ya kusikia kelele zikipogwa kutoka kwa watoto hao.


Moto huo ambao umesebabishwa na kibatali umeteketeza nyumba nzima pamoja na mali zote, ikiwemo vifaa vya shule vya wanafunzi hao walionusurika,pamoja na kukuta baadhi ya viungo vya mtoto  aliyepoteza maisha vikiwa vimeteketea kabisa kwa moto.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo