Msemaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Christopher Ole Sendeka
amesema Edward Lowassa ni muungwana na kwamba asingeweza kuacha kumsalimia kwa
kumpa mkono Rais John Magufuli.
Ole Sendeka amesema jana:
“Namfahamu Lowassa ni muungwana hawezi kuacha kusalimiana
kwa kupeana mkono na Rais. Wamekutana viongozi, Rais na waziri mkuu mstaafu hawawezi
kuacha kusalimiana.”
Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema aliyechuana na Rais Magufuli katika
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015 mwaka jana, juzi walikutana kwa mara ya kwanza na
mpinzani wake huyo tangu kinyang’anyiro hicho kilipomalizika.
Viongozi hao walikutana kwenye misa ya jubilei ya dhahabu ya ndoa ya Rais mstaafu, Benjamin
Mkapa na mkewe Anna katika Kanisa la Mtakatifu Petro.