Maneno kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Iringa "jana saa 3 na dakika 25 Usiku nilipokea wakina mama 3 wakiwa wanatetemeka
kwa baridi, wakilalamika kumwagiwa maji walipokuwa wamekaa kwenye eneo
la kusubiria wagonjwa walio lazwa hasa kwa wale walio toka mbali.
Maji
hayo yalimwagwa na walinzi wa kampuni ya Amazon ambao ndio wamepewa
kandarasi ya ulinzi hospitali ya Rufaa ya Iringa.
Nilifika hospitali
kujionea mwenyewe hali halisi, baadae nikapata taarifa kuwa jana yake
Mlinzi alimpiga mzee aliyekuwa ameleta chakula hospitali na kumwaga kwa
mateke.
Niliamuru mlinzi huyo na mwenzake wakamatwe pia mwenye kampuni
afike kituo cha polisi haraka iwezekanavyo.
Hali hii imeudhi sana hasa
ukiona jinsi wakina mama walivyo nyanyasika wengine vyombo vyao na
chakula kuroweshwa maji."













