Jambo jema Kwa Makete lililosemwa na mbunge Norman Sigala

 Mbunge wa jimbo la Makete Mh Prof Norman Sigala King
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Bw. Deo Sanga



Wilaya ya Makete ni miongoni mwa wilaya chache zitakazokuwa za kwanza kupata mgawo wa madawati yaliyotolewa na serikali kuu hivi karibuni

Hayo yamebainika katika siku ya pili ya ziara ya Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Bw. Deo Sanga yenye lengo la kukagua utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi katika wilaya ya Makete

Akiwa kijiji cha Ilevelo kata ya Lupalilo wilayani Makete mwenyekiti huyo amewasisitiza wananchi hao kushirikiana na viongozi wao kuleta maendeleo, na ameyasema hayo mara baada ya kupokea taarifa na kukagua ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho

Diwani wa kata ya Lupalilo Mh Imani Mahenge nae amesoma taarifa ya ujenzi wa zahanati hiyo

Naye Mbunge wa jimbo la Makete Mh Prof Norman Sigala King amewatoa hofu wananchi hao kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo elimu kwa kusema kwamba zaidi ya madawati 500 yametolewa na serikali kwa ajili ya shule za wilaya ya Makete na yatafika hivi karibuni


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo