Mauaji ya kutisha na ya kikatili yameendelea kutikisa Wilayani Makete Mkoani Njombe kufuatia Usiku wa kuamkia jana mtu aliyefahamika kwa jina la Efwadi Mahenge (38) mjasiriamali, kuuawa kwa kukatwa shingo na kitu chenye ncha kali kijiji cha Isapulano Wilayani Makete
Mauaji hayo yametokea usiku wa kuamkia jana eneo la Mpoma karibu na inapojengwa Shule ya sekondari Isapulano ambapo mauaji hayo yanadaiwa kufanyika
Tukio hilo linahusishwa na Wivu wa Kimapenzi ambapo inadaiwa kuwa Marehemu alikuwa akijihusisha Kimapenzi na mke wa Mtu japo taarifa hizo bado hazina uthibitisho, na Wananchi wa kijiji hicho wamekemea matukio hayo na kuwataka wananchi wenzao kufuata sheria na taratibu wanapogundua kuwa kuna njia mbaya zinazoweza kuhatarisha Maisha ya mtu, huku wakisema kuwa wanakosa Amani kuhusu uwepo wa tukio hilo la Kinyama
Albat Mahenge Katibu wa kitongoji cha Stendi alikuwa katika zoezi la kutafuta Mwili wa Marehemu ambaye hakuonekana tokea juzi Agosti 13 lakini asubihi ya jana wakaanza kumtafuta na ndipo walipoukuta mwili wa Marehemu umeharibika usoni na inaonekana alipigwa na Fimbo tumboni na kukatwa shingo

Mwenyekiti wa kijiji cha Isapulano Mwatindi Mbilinyi amesema Matukio hayo yanaashiria hali mbaya kijiji hapo lakini amewaasa wananchi kutojichukulia sheria mkononi na badala yake wanapojua kuwa kuna Dalili au ugomvi basi watoe taarifa katika eneo husika ili kuzuia mauaji
Kaka wa Marehemu Oswad Mahenge amekemea Tukio hilo na kuwaomba ndugu zake kuwa na moyo wa Uvumilivu kwa muda huu ambao Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kumtia nguvuni mtu au watu waliohusika na Mauaji hayo
Jeshi la polisi limefika kijijini hapo na kushuhudia tukio hilo la kikatili ambapo mpaka tunakwenda mitamboni hakuna mtu anayeshikiliwa kwa tuhuma za mauaji hayo na upelelezi wao unaendelea, huku Jeshi hilo likiwataka wananchi kutoa ushiriakiano wa kuwakamata watuhumiwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria