CHADEMA Watangaza kuandamana Makete Nzima

Na Fadhili Lunati
Chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) wilaya ya Makete kimesema kimejipanga kushiriki maandamano na mikutano ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono maazimio ya kamati kuu ya chama hicho juu ya oparesheni UKUTA iliyopangwa kufanyika Septemba Mosi mwaka huu.


Akizungumza nasi Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA wilaya ya Makete Bw.Ibrahim Ngogo ameelezea maandalizi hayo.

Aidha Bw.Ngogo ameelezea hali ya demokrasia nchini na pamoja na haki na wajibu wa vyama vya siasa vilivyosajiliwa kwa mujibu wa sheria.

Pamoja na kuelezea kwa kile alichodai kuwa ni kuminywa kwa demokrasia Bw.Ngogo amesema anatambua utendaji kazi wa Rais Magufuli huku akibainisha kuwa angeruhusu uhuru wa vyama vya siasa kutekeleza majukumu yake anaamini kuwa angeweza kufanya vizuri zaidi.

Aidha Bw.Ngogo ameelezea namna watakavyotekeleza mpango huo kwa wilaya ya Makete huku akibainisha kuwa watafanya mikutano na maandamano kuanzia ngazi ya vijiji kuelekea kutoka ofisi za chama kuelekea katika ofisi za serikali.

SIKILIZA SAUTI HAPA CHINI:-


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo