Habari za kusikitisha zimetufikia muda huu kuwa malkia wa Tarabu nchini
Bi. Shakila Saidi amefariki dunia jioni ya leo muda mfupi baada ya
kuanguka na kukimbizwa hospitali ya karibu na nyumbani kwake Mbagala
Charambe jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika
vilivyo karibu na marehemu, Bi Shakila hakuwa anaumwa ila alianguka
ghafla na alipofikishwa hospitali akakata roho.