Hii imeripotiwa na kituo cha Televisheni cha kimataifa cha CCTV Africa kuwa kwenye hifadhi ya Taifa ya Tarangire ambayo iko kusini
magharibi mwa Arusha Tanzania. Wakazi wa maeneo jirani na mbuga hiyo
wamebuni njia ya kufukuza wanyama ili wasiharibu mazao yao na kuwafukuza
mbali na makazi yao.
Unaambiwa
wamekuwa wakitumia Kondomu kuzuia wanyama kama tembo kuharibu
mazao. Imeelezwa kuwa wanatumia unga wa pilipili na kondomu kufukuza
wanyama waharibifu.
Njia hii imeelezwa kufanya kazi vizuri na pia
imekuwa ikisaidia wanyama kutopata madhara.
Unaweza kuangalia kipande cha video hapa chini