Ufafanuzi wa Serikali kuhusu Madawati Mengi Makete, Sikiliza Sauti hii

Halmashauri ya wilaya ya Makete mkoani Njombe imelazimika kutoa ufafanuzi wa nyongeza ya madawati iliyoripotiwa wilayani hapo ili hali wapo wananchi wanaoendelea kuchangia madawati katika shule zilizopo katika vijiji vyao

Ufafanuzi huo umetolewa na Afisa elimu Msingi wilaya ya Makete Mwl. Antony Mpiluka wakati akizungumza nasi baada ya kuwepo malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya wananchi kuwa imetolewa taarifa ya ongezeko la madawati ilihali vipo baadhi ya vijiji vinavyoendelea kuchangia madawati

Mwl Mpiluka amesema madawati yaliyozidi yanatokana na maeneo mbalimbali ya wilaya ya Makete kuchangia fedha za madawati kutokana na kuitikia wito wa serikali, hivyo ni ngumu kwa madawati yaliyozidi kwenye kijiji kimoja kupelekwa kwenye kijiji kingine kwa kuwa madawati hayo ya akiba ya eneo moja yaliyozidi yanatunzwa kwa matumizi ya baadaye

Hata hivyo amewataka wananchi kuchangia madawati katika maeneo yao bila kuangalia kama yatazidi kwa kuwa ziada hiyo ya madawati itawasaidia katika matumizi ya baadaye kwa kuwa elimu inazidi kukua siku hadi siku

Msikilize Mwl Mpiluka akiongea na sisi hapa chini:-


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo