Halmashauri ya wilaya ya Njombe Mkoani Njombe imetangazwa mshindi wa jumla kwenye usafi wa mazingira nchini na kukabidhiwa Gari baada ya takwimu kuonesha halmashauri hiyo kutokuwa na mgonjwa hata mmoja aliyekumbwa na ugonjwa wa kipindupindu
Kwa mujibu wa wizara ya afya ushindi huu unaashiria kwamba Njombe imefanya vizuri zaidi mbele ya majiji manispaa na halmashauri nyinginezo nchini
Valentino Hongoli ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe ameeleza mikakati iliyofanikisha wao kuibuka kidedea kuwa ni pamoja na wataalamu wake kupita vijijini kuelimisha wananchi juu ya utunzaji wa mazingira
Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummi Mwalimu ameelezea vigezo vilivyoangaziwa katika ushindani huo ambapo miongoni mwa vigezo hivyo ni matumizi ya vyoo bora
Sikiliza Sauti hii