Mchango wa wananchi waokoa Jahazi Shule ya Msingi Tandala (Audio)

Wanafunzi wa shule ya msingi Tandala Mazoezi  iliyopo katika kata ya Tandala wilayani Makete mkoani Njombe wamewashukuru wananchi kwa mchango wao wa madawati walioutoa na kufanikisha kukamilika kwa baadhi ya madawati.
 
Radio Green fm kupitia kwa mwandishi wake Godfrey Martin imefika katika eneo la utengenezaji wa madawati hayo na kushuhudia Nyuso za wanafunzi zilizojawa na furaha baada ya idadi ya madawati kuongezeka shuleni hapo na kusema kuwa kutokana na uchache wa madawati walilazimika kukaa zaidi ya wanne kwenye dawati moja huku wakitoa ahadi ya kuyatunza madawati hayo.

Naye Mwalimu mkuu msaidizi wa Shule hiyo Bw. Zacharia Mtewele Mbali na kuthibitisha kukabidhiwa madawati hayo amekiri kuwepo kwa uhaba wa madawati katika shule yake na kuweka bayana moja ya mkakati utakaosaidia madawati hayo kudumu

Onesmo Sanga ni Fundi seremala aliyepata zabuni hiyo na hapa ameongelea vipimo alivyotumia kutengeneza madawati hayo pamoja na idadi ya wanafunzi wanaotakiwa kukaa kwenye Dawati moja.

Naye mwenyekiti wa kijiji cha Tandala Bw. Andowise Memba ameelezea jitihada zilizotumika kufanikisha kukusanya fedha kutoka kwa wananchi na kuwashukuru kwa hatua waliyoifikia ya Kupatikana kwa madawati 20 yaliyogharimu Fedha za kitanzania shilingi milioni moja na laki mbili licha ya kuwa lengo lao ni kupatikana kwa madawati Arobaini.


Na Godfrey Martin

sikiliza sauti hizi hapa chini


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo