Wenyeviti wa vitongoji vitano katika kijiji cha Usagatikwa kilichopo kata ya Tandala Wilayani Makete mkoani Njombe wanadaiwa kuchangia kukwama kwa shughuli za maendeleo katika kijiji hicho.
Wakizungumza na mwandishi wetu wakati wa utekelezaji wa shughuli za maendeleo kijijini hapo mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Albeto Sanga na afisa mtendaji wake Bw. Ayubu Sanga wamesema kuwa Wananchi hawakutojitokeza kwa wingi katika zoezi la kubeba mbao kijijini hapo
Wamesema kuwa wanawachukulia hatua wanaokiuka lakini wakifikishwa kwenye baraza la kata wanaachiwa huru na kupandikiza chuki kwa wananchi wenginehuku baadhi ya wananchi wa kijiji cha Usagatikwa wakizungumzia kuhusiana na suala la maendeleo kijijini hapo.

Afisa mtendaji wa kata ya Tandala Bi Karmela Maley anawasihi viongozi katika kata hiyo kuwa kitu kimoja ili kufanikisha suala hilo la maendeleo.
Kituo hiki kimeshuhudia wananchi watano tu ambao wamejitokeza katika siku ya maendeleo kijijini hapo kati ya wakazi wote waliopo na jitihada za kuwapata wenyeviti hao wa vitongoji zimekwama baada ya kutopatikana katika simu zao za mikononi na hawakuwepo kwenye shughuli hizo za maendeleo.

Na Asukile Mwalwembe
Sikiliza sauti hizi hapa chini