Baraza
la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, limekifutia usajili wake wa kutoa
huduma za kitabu, Kituo cha Tiba Asilia cha ForePlan Kliniki iliyopo
Ilala Bungoni jijini Dar es salaam, kinachomilikiwa na Dkt. Juma Mwaka
maarufu kama Dkt. Mwaka, kwa madai kuwa kimekiuka taratibu za kitabu za
tiba asili huku akiwa ameonywa na kushindwa kubadilika.
Akizungumza
jijini Dar es salaam leo katika Mkutano na waandishi wa habari,
Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dk. Edmund Kayombo amesema kuwa kufutiwa
kibali cha Dk. Mwaka kunatokana na sababu nyingi ambazo amekuwa akikiuka
licha ya kupewa maonyo na barua juu ya utoaji huduma zake.
Amesema sababu nyingine ni kuwa katika matangazo yake amesema anatoa tiba za kisasa wakati hiyo elimu hana ya kufanya hivyo.
Wengine
waliofutiwa usajili ni Fadhaget Sanitarium kinachoendeshwa na Tabibu
Fadhili Kabujanja pamoja na Mandai Herbal Clinic kinachoendeshwa na
Tabibu Abdallah Mandai.
Hata
hivyo limetoa adhabu mbalimbali kwa kituo cha Aman Herbal Clinic
kinachoendeshwa na Tabibu Esbon Baroshigwa, na Tabibu Castory Ndulu wa
Kituo cha Ndulu Herbal Clinic wamepewa barua ya onyo.
Aidha
wengine wamesimashwa kwa miezi sita ambao ni Tabibu John Lupimo wa
Lupimo Suntarium Herbal Clinic pamoja na Tabibu Simon Rusigwa wa Sigwa
Herbal Clinic.
Dk.
Kayombo amesema kuwa wale wote ambao wamepewa onyo pamoja na
kusimamishwa wametakiwa wasiingie mikataba na vyombo vya habari kwa
ajili ya Matangazo.
Amesema
kuwa waliofutiwa walifuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kuwahoji na
kujiridhisha kuwafutia kibali cha utoaji wa huduma za tiba asili na
tiba mbadala.