Maige aliyeshika nafasi ya unaibu waziri mwaka 2008 hadi
2010 akiwa na Waziri Shamsa Mwangunga na kisha kuwa waziri kamili
kuanzia Novemba 27, 2010 hadi Mei, 2012, alisema hadi wakati akijiuzulu,
alisema ushahidi wa anachokisema ni ukweli kuwa hakuna mahala alikopewa
nafasi ya kujieleza kuhusiana na tuhuma hizo.
Alisema cha kusikitisha, ni ukweli kwamba hatua za
kumuwajibisha zilichukuliwa kutokana na mazingira ya wakati huo ya
“kufuata upepo” unakovuma na pia kunyimwa kwake fursa ya kujieleza
bungeni na aliyekuwa Spika wa Bunge la 10, Makinda.
Alisema kutokana na yote hayo, ndipo alipojikuta akipoteza
uwaziri na hadi sasa amebaki na siri nzito moyoni kuhusiana na mambo
hayo na pia vitendo vya ujangili.
Maige aliondolewa uwaziri na Rais Kikwete baada ya taarifa
ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, kumtuhumu kuwa
alihusika katika kugawa vitalu vya uwindaji kwa kampuni hewa 16.
Aliponzwa pia na uuzaji wa wanyama hai wakiwamo twiga.
"Bahati mbaya, sisi tuliosimamia sheria tuliondolewa kwa
hila. Na bahati mbaya, kwa mazingira ya wakati ule, upepo ukivuma sana
unakwenda hivyo hivyo… Ila hivi sasa (chini ya Rais John Magufuli) mambo
yamebadilika… kuna usimamizi wa sheria," alisema Maige.
MAKINDA ALIVYOMPONZA
Akielezea kile kilichotokea kabla ya kuachia uwaziri, Maige alisema Makinda alishiriki kwa kiasi kikubwa katika kuondolewa kwake uwaziri kutokana na kile anachodai kuwa spika huyo mstaafu alimkandamiza kwa kutompa muda wa kujitetea bungeni baada ya tuhuma kadhaa kuelekezwa kwake kuhusiana na ugawaji wa vitalu vya uwindaji.
Akielezea kile kilichotokea kabla ya kuachia uwaziri, Maige alisema Makinda alishiriki kwa kiasi kikubwa katika kuondolewa kwake uwaziri kutokana na kile anachodai kuwa spika huyo mstaafu alimkandamiza kwa kutompa muda wa kujitetea bungeni baada ya tuhuma kadhaa kuelekezwa kwake kuhusiana na ugawaji wa vitalu vya uwindaji.
Alisema kabla ya kuondolewa, aliomba apewe fursa ya kuelezea
ukweli wa suala hilo, lakini kwa bahati mbaya mazingira kuhusiana na
jambo hilo yalijaa harufu ya rushwa na hujuma zilienea dhidi yake hadi
bungeni ambako mwishowe hakupata nafasi hata ya kusikilizwa.
"Nilisema bungeni kwamba jambo lolote linalowasilishwa
bungeni ni lazima liwe limepitia kwenye kamati. Na huko kwenye kamati ni
lazima majadiliano yawe yamekamilika… nilisema yote yaliyojadiliwa
bungeni sikuwahi kuitwa na kamati kujibu tuhuma zinazoelekezwa,"alisema
Maige na kuongeza:
"Bungeni nikasema, Mheshimiwa Spika, utaratibu hauruhusu
hili jambo kujadiliwa maana sijaitwa kwenye kamati… lakini Spika kwa
sababu alikuwa na vionjo vyake, ana malengo yake, alisema kamati
inaruhusiwa kufanya kazi kama inavyopenda, wewe changia kama
mchangiaji.”
Maige aliongeza kuwa baada ya hapo, alifanya jitihada za
kuzungumza na mawaziri wenzake, hasa aliyekuwa akishughulikia Sera,
Uratibu na Bunge ili asaidiwe kupata nafasi ya kutosha ya kujieleza
bungeni lakini jitihada zake hizo pia hazikufanikiwa.
"Nikasema tena na mawaziri wenzangu, nikimzungumzia Waziri
wa Sera, Uratibu na Bunge, nikamwambia usimame usaidie hili suala maana
mimi hapa sizungumzi kama Maige, ninazungumza kama Waziri wa Serikali…
naomba uliombe Bunge lisitishe mjadala ili nikaandae majibu kama Waziri.
Nilipewa dakika 10 za kuchangia kama mchangiaji wa kawaida," alisema.
"Sijaona Waziri, tena mlengwawa tuhuma, anachangia kwa
dakika kumi. Zimekuja skendo za ajabu ajabu kama Escrow, Waziri husika
amepewa zaidi ya saa moja na dakika 20, anaeleza msimamo wa Serikali.
Lakini mimi nilipewa dakika kumi, nilijaribu kueleza (lakini) muda
sikupata,"alisema.
chanzo: nipashe
