Kambi rasmi ya upinzani bungeni
imewasilisha hoja maalumu ya kumuondoa madarakani Naibu Spika wa Bunge
la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson kwa kile wanachodai
amekuwa akiliendesha Bunge hilo kwa ubabe dhidi ya wabunge wa kambi
rasmi ya upinzani bungeni huku wakiainisha sababu sita zikiwemo za
matumizi mabaya ya sheria za kanuni za uendeshaji wa Bunge.
Miongoni mwa sababu hizo sita walizowasilisha mezani kwa Spika wa
Bunge ni pamoja na Dkt Tulia Ackson, kuweka maslahi ya chama mbele
kuliko maslahi ya Bunge, matumizi ya mabaya ya kiti cha spika,
ukiukwaji wa kanuni ya 64,1, f na g, inayokataza mbunge kutumia lugha ya
matusi, huku ikisisitiza kuwa ombi hilo limekwisha kuungwa mkono na
wabunge 92 kwa niaba ya wabunge wengine.
Zikiwa ni takribani siku nne, kambi hiyo ya upinzania ikiwa
haishiriki vikao vya bajeti,wabunge kutoka chama tawala CCM, wanasema ni
vema mazungumzo yakafanyika.
Katika kipindi cha maswali na majibu wabunge wameihoji serikali kuhusu utekelezaji wa mipango mbalimbali ikiwemo ya miundombinu.