JESHI
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewataka wenyeviti wa
serikali za mitaa kushirikiana na wenye nyumba kuhakikisha wapangaji
katika nyumba wanaingia makubaliano ya mkataba na kuwa na picha zao.
Hatua
hiyo imetokana na kuwepo kwa watu wanaofanya uhalifu katika maeneo
mbalimbali na kushindwa kupatikana pindi polisi wafanyapo operesheni
kutokana na kupanga kwenye nyumba hizo lakini wakati akiondoka hawaagi
na wenye nyumba wanakosa kuwa na taarifa za watu katika nyumba zao.
Akizungumza
na waandishi habari jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi wa
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina (CP), Simon Sirro amesema kuwa
wenye nyumba ambao watashindwa kufanya mkataba bila picha likitokea
tukio dhidi ya mpangaji msalaba utamuangukia mwenye nyumba kuhusika
katika uhalifu uliofanywa.
Wakati
huohuo Jeshi la Polisi linamshirikia Askari wa Jeshi la Wananchi
(JWTZ), MT 66807 SGT, George Kwisema kwa tuhuma za kukutwa na vipande
kumi vya meno ya tembo vyenye thamani ya Sh. milioni 198 vikiwa katika
gari yake yenye namba za usajili T.477 AXS aina ya Suzuki Vitara.
Katika
tuhuma za vipande vya meno ya tembo wanaoshikiriwa wengine, ni Shafi
Muhibu pamoja na Asha Hassan ambao walikutwa katika gari iliyokuwa
imebeba meno ya tembo.
Wakati
huo huo, Jeshi la Polisi linawashikiria watu watatu kwa tuhuma za
kukutwa na sukari mifuko 35 ya Kilogram 50 ambao walikamatwa Chadibwa
Mtaa wa Magogoni Kigamboni Mei 31 mwaka huu, ambayo ilikuwa haijalipiwa
ushuru na waliokamatwa na tuhuma za sukari ni Said Bakari (25), Mkazi wa
Mbagala , Hamadi Selemani pamoja na Bakari Masudi.
Jeshi
la Polisi linafanya upelelezi pia wa mtuhumiwa wa aliyewaleta wahamiaji
Haramu na kutoweka katika mazingira ya utatanishi akiwa chini ya ulinzi
wa Polisi.