Vigogo watumbuliwa kwa kusafiri nje ya nchi bila kibali

Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amewasimaisha kazi kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Kibaha Leah Lulanji pamoja na afisa utamaduni wa mji huo Abdul Haufi kwa tuhuma za kusafiri nje ya nchi bila kibali, ikiwa ni kukaidi agizo la Rais John Magufuli

Akizungumza mara baada ya kutembelea shule za msingi kukagua zoezi la utengenezaji madawati, Ndikilo amesema amewasimamisha kazi watumishi hao kwa kosa la kusafiri kwenda nchini Sweeden bila kuomba kibali kutoka ngazi yeyote jambo ambalo ni ukiukwaji wa waraka namba 13 uliotolewa na ofisi ya rais Tamisemi, Huku akiiagiza halmashauri ya KIbaha kumpelekea kwa maandishi kiasi cha fedha ambacho halmashauri imetumia kugharamia safari hizo

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa amemvua nafasi ya Ualimu Mkuu mwalimu mkuu wa shule ye msingi Mailimoja Sedekia Fanuel kwa kosa la kuchelewa kuingia kazini pamoja na kosa la kuruhusu wanafunzi kutumikishwa na walimu kwa kufanya kazi ya kuwapikia chai walimu hao na kuacha masomo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo