Anusurika kupewa likizo ya siku 14 ya ndoa

Mkazi mmoja wa Kata ya Osunyai, Mtaa wa JR, amesurika kupewa adhabu ya mapumziko ya ndoa yake kwa siku 14 na uongozi wa mtaa kwa kosa la kushindwa kuwa makini na malezi ya mtoto wake wa kambo.
Wazo hilo lilitolewa na mwenyekiti wa mtaa wa JR ,Ezekiel Mollel baada ya kuonekanika mama huyo kuwa mzembe kwenye malezi ya mtoto wake wa kambo na kusababishwa kuwa na alama nyingi za kuchapwa na fimbo aina ya mjeledi sehemu kubwa ya mwili wake aliyokuwa anachapwa msichana wa kazi.
"Huyu mama ni mzembe ,haiwezekani watoto wake wasichapwe na kuumizwa hivi lakini huyu wa kambo awe hivyo, hata kama ni kazi ,ilipaswa amjue na huyu mtoto hali yake,"alisema Ezekiel.
Wazo hilo lilipingwa na mwenyekiti wa mtaa wa 'Kirika B' Christopher Salivatory baada ya kuona kamati na uongozi wa mtaa ulishampa masharti ya kuhakikisha anakuwa makini na mtoto huyo ambaye ametolewa taarifa na majirani kuwa ananyanyaswa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo