Hiyo inafuatia Tukio la kikatili lililotokea usiku wa kuamkia jana katika kijiji cha Usungilo kata ya Mang’oto wilayani Hapa ambapo wananchi wenye hasira kali wamemuua kwa kumchoma moto Bw. Silvester Mbilinyi anayekadiriwa kuwa na miaka 25 kwa tuhuma za wizi
Tukio hilo la kusikitisha limekuwa ni mfululizo wa Matukio mabaya zaidi kutokea wilayani Makete kwa kipindi cha Mwezi huu
Hamfrey Msigwa mtendaji wa kijiji cha Usungilo amesema mtuhumiwa huyo alibomoa vibanda vya biashara vya watu watatu mnamo tarehe 21 June 2016 na anaelezea tokea kuanza kwa tukio mpaka mwishowe umauti unamkuta mtuhumiwa
Daktari kutoka Hospitali ya wilaya ya Makete Idrisa Kilanga amethibitisha mauaji hayo na kusema kwamba aliyekufa ni wa Jinsi ya Kiume na amechomwa moto huku sura yake haijulikani vizuri kutokana na kuungua vibaya
Jeshi la polisi limefika eneo la tukio mnamo saa 12:00 jioni ya jana na kushuhudia majivu mahali mauaji yalipotokea jirani na ofisi ya Afisa Mtendaji wa kijiji cha Usungilo na kwenda Makaburini kuona mwili wa Marehemu aliyeunguzwa vibaya na kutoa wito kwa Raia kutojichukulia sheria Mkononi kwani hali hiyo inasababisha kuvurugika kwa Amani Wilayani Makete
Sikiliza sauti hapa chini
