Mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Bw.Fransic Namaumbo wakati
akizungumza moja kwa moja kupitia kituo cha redio Green Fm
Wito umetolewa kwa wananchi wa wilaya ya Makete mkoani Njombe kujitokeza kwa wingi katika shamrashamra za kuupokea mwenge wa uhuru unaotarajiwa kuwasili wilayani Makete Alhamisi Juni 16 mwaka huu.Wito huo umetolewa Jana na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Bw.Fransic Namaumbo wakati akizungumza moja kwa moja kupitia kituo cha redio Green Fm.
Bw. Namaumbo amesema kuwa mwenge huo wa uhuru utapokelewa wilayani Makete katika kata ya Mbalatse ukitokea katika halmashauri ya Njombe Mji na ukiwa ndani ya wilaya ya Makete utazindua na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo.
Hata hivyo mkurugenzi ameelezea manufaa ya mwenge huo kufika Makete licha ya kutembelea miradi mbalimbali kuwa ni pamoja na kuleta mshikamano
Mwenge wa uhuru utakabidhiwa tarehe 17 mwezi huu katika halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe.
Na Erica Mbilinyi