Akizungumza kwa njia ya simu na blog hii mganga mkuu wa wilaya ya Makete .Dr Joseph Gasper Kimaro amesema licha ya zoezi la uchangiaji wa damu salama kuanza tangu siku ya wauguzi duniani iliyofanyika Mei 12 mwaka huu, bado mwitikio ni mdogo kutoka kwa wachangiaji wa damu.
Amesema kuwa hali hiyo huwenda inatokana na kutofanywa uhamasishaji na utoaji wa elimu ya uchagiaji damu salama kwa wakazi wa wilaya ya Makete huku akisema hivi sasa wanatarajia kuanza kufanya hamasa ya uchangiaji wa damu salama kwa baadhi ya kata za wilaya ya Makete.
Dr. Kimaro amesema kuwa hakuna madhara kwa wanaochangia damu kama baadhi ya watu walivyoaminishwa na kusema kuwa hivi sasa huduma hii inapatikana hospitali ya wilaya ya Makete.
Hata hivyo amewataka wananchi kutambua kuwa kila mmoja hajui siku ambapo atahitaji kuongezewa damu, hivyo ni vyema kushiriki kuchangia damu ambapo zoezi hilo kwa hospitali ya wilaya ya Makete linafanyika siku ya Jumatatu hadi Alhamisi kila wiki.