Kutokana na hamasa zilizotolewa na ujio wa Mwenge wa Uhuru wilayani Makete mkoani Njombe Juni 16 mwaka huu, katika usiku wa mkesha wa mwenge wananchi wamejitokeza kwa wingi kupima virusi vya UKIMWI kwa hiari na saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake, huku baadhi wakikutwa na maambukizi ya VVU
Takwimu hizo zimetangazwa hivi karibuni katika uwanja wa Mkesha stendi mpya Tandala na Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Daudi Yassin ambapo baada ya kutangazwa mkazo pia ukatolewa na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa George Mbijima
Matokeo ya VVU na Saratani ya shingo ya Kizazi Makete baada ya Mkesha wa Mwenge (Audio)
By
Edmo Online
at
Monday, June 20, 2016