Afisa mazingira wilayani Makete mkoani Njombe Bwana Rafaeli Kalongola amesema kuwa tangu waanze kutoa elimu juu ya utunzaji wa mazingira Wilayani Makete maendeleo yake ni mazuri kutokana na wananchi kuipokea elimu hiyo hususani katika suala la uchomaji moto ovyo kunakopelekea kuharibu mazingira
Bwana Kalongola amesema kuwa tatizo la uchomaji moto mazingira wilayani Makete limepungua kwa kiasi kikubwa huku akiwataka watendaji wa kata kuchagua maeneo maalumu kwa ajili ya kutupa takataka ngumu zinazotokana na vinywaji mbalimbali pamoja na mifuko ya plastiki maarufu kama rambo.
Kwa upande mwingine Bwana Kalongola amewataka wananchi wilayani Makete kutopanda miti kwenye maeneo ya mashamba yenye rutuba kwa ajili ya mazao ya kilimo huku akitoa wito kwa kila kijiji kufanya mipango ya kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya kupanda miti na mengine kwa shughuli za kilimo
Aidha amesema kuwa wana mpango wa kukutana na wadau mbalimbali nje ya wilaya hii wanaonufaika na vyanzo vya maji vya Makete ili wawe wanachangia jitihada za utunzaji mazingira katika wilaya ya Makete