Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Dokta Asumpta Mshama
Na Gabriel Kilamlya.
Watumishi Wanne wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Akiwemo Mkuu wa Idara Hiyo Michael Haule Wamesimamishwa Kazi Baada ya Kuandika Taarifa ya Uongo Juu ya Vikundi Vya Vijana na Wanawake Waliopaswa Kupatiwa Mikopo Siku ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2016.
Hatua Hiyo Imechukuliwa na Mkuu wa Wilaya Hiyo Dokta Asumpta Mshama Baada ya Kulazimika Kwenda Kukagua Vikundi Hivyo Ambavyo Vilionekana Kukosa Sifa Mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka Huu Bwana George Mbijima Ambaye Aligoma Kukabidhi Hundi ya Shilingi Milioni 51 Kwa Vikundi Zaidi ya 200 Hapo Juni 17 Mwaka Huu Kupitia Fedha ya Halmashauri Inayotengwa Kwa Asilimia 5 ya Mapato ya Ndani.
Aidha Udanganyifu Mkubwa Umebainika Wakati wa Uhakiki Huo Aliofanya Katika Vijiji Vya Igwachanya Ambako Amefuta Kikundi Hicho,Luduga,Usuka,Ujange na Banawanu Ambako Pia Amebaini Kuwepo Kwa Vikundi Vya Vijana Ambao Wana Umri wa Miaka Hadi 60 Ilihali Muongozo wa Kupata Fedha Hizo Unawataka Vijana Wenye Umri wa Miaka 18 Hadi 35.
Udanganyifu Huo Umeonekana Kumkasirisha zaidi Mkuu Huyo wa Wilaya Dokta Mshama na Kulazimika Kutangaza Kuwasimamisha Kazi Watumishi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Waliohusika na Kuunda Vikundi Hivyo Kwani Amesema Aliomba Majina ya Vikundi Hivyo Siku Nyingi Lakini Hakupewa Hadi Walipoumbuka Siku ya Mwenge wa Uhuru .
Aidha ametaka zoezi hilo kufanyika upya ndani ya mwezi mmoja na Wataalamu watafutwe wengine katika kipindi cha Wiki Mbili kwa ajili ya kazi hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri Hiyo Melkizedeki Humbe Ameonekana Kushangazwa na Kitendo Cha Watumishi Hao Kuandaa Taarifa ya Uongo Kwani Alishaidhinishi Shilingi Milioni Mbili Kwa Ajili ya Kwenda Kuhakiki Vikundi Hivyo Tangu Siku Nyingi.
Akizungumza Wakati wa Tathmini ya Ziara Hiyo ya Mkuu wa Wilaya Pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama Iliyokwenda Vijijini Humo Kuhakiki Vikundi Hivyo Ikiongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri Hiyo Mkuu wa Idara Hiyo Aliyesimamishwa Kazi Ameonekana Kuwa na Maelezo ya Kujikanganya Wakati Akihojiwa na Mkuu wa Wilaya.