Kijiji cha Masisiwe Makete chafanya Uamuzi wa Kuigwa (Audio)

Wananchi wa kijiji cha Masisiwe kata ya Ukwama Wilayani Makete mkoani Njombe wamefanikiwa kujenga vyoo bora  kwenye nyumba za  walimu kwa kushirikiana na serikali ya kijiji hicho.

Hayo yamebainishwa na Afisa mtendaji wa kijiji hicho Bw.Danford Sanga wakati akizungumza na mwandishi wetu.

Amesema kuwa ujenzi huo ulianza mapema mwaka huu na kila mwananchi alichangia kiasi cha shilingi elfu tano na kila choo kiligharimu kiasi cha shilingi milioni moja na laki tano.

Bw. Sanga amaeiomba serikali iwasaidie ili waweze kukamilisha ujenzi huo.

Pia amewapongeza wananchi wa kijiji cha Masisiwe kwa kujitoa kujenga vyoo hivyo bora vya walimu na kuwaomba  wale ambao bado hawajajenga vyoo bora nao wajenge katika nyumba zao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo