JWTZ Yakanusha Taarifa za Kuibwa kwa Kifaru.....Lasema Hakuna Ukweli Wowote

Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ)  limekanusha taarifa za kuibiwa kwa kifaru  cha jeshi zilizoripotiwa leo na gazeti la Dira  na kusema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote huku  likisisitiza ulinzi katika maeneo ya jeshi uko imara.

Akiongea na  waandishi wa habari leo  kukanusha habari hizo, msemaji wa jeshi hilo, Kanali Ngemela Lubinga amesema jeshi limesikitishwa sana na habari hizo za upotoshaji kwa kuwa zinachafua taswira ya jeshi na taifa kwa ujumla.
 
Amelitaka Gazeti la Dira kuomba radhi mara moja na wakishindwa kufanya hivyo hatua Kali na za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao 

==>Zaidi, tazama video hii kumsikiliza


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo