Polisi apiga maafisa wa kampuni ya udalali

Zoezi la kuwaondoa kwenye nyumba za serikali wadaiwa sugu linalofanywa na wakala wa majengo (TBA) mkoa wa Mwanza kwa ushirikiano na kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart, limeingia dosari baada ya mmoja wa wapangaji wa nyumba hizo eneo la Mkuyuni A, jijini Mwanza kutembeza mkong’oto uliosababisha zoezi hilo kusitishwa.

Zoezi hilo lililokuwa likisimamiwa na askari polisi wawili wenye silaha, limeingia nuksi baada ya mpangaji huyo ambaye ni askari polisi wa kitengo cha upelelezi wilaya ya Nyamagana Fabian Jumapili kufika nyumbani kwake akitumia Defender ya polisi na kuanza moja kwa moja kutembeza kipigo kwa wafanyakazi wa kampuni ya Yono Auction Mart ambao walikuwa wakiendelea na kazi ya kutoa nje vyombo vyake vya ndani.
 
Miongoni mwa watu walioshuhudia tukio hilo lililotokea majira ya saa sita mchana ni Bi. Esther Joseph na Asha Omar ambao wameeleza changamoto za utekelezaji wa zoezi hilo.
 
Afisa wa kampuni ya Yono Auction Mart, Habariki Mhina ambaye amejeruhiwa mdomoni wakati wa vurugu hizo amesikitishwa na kitendo kilichofanywa na mpangaji huyo.
 
Mhandisi Sobe Makonyo ni Kaimu Meneja wa wakala wa majengo mkoa wa Mwanza anaeleza hatua zitakazochukuliwa mara ya baada ya mdaiwa huyo kukaidi agizo la serikali kwa kuanzisha vurugu zilizopelekea kusitishwa kwa zoezi hilo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo