Taarifa
hizo zinazosambazwa, pamoja na mambo mengine, zinaeleza kuwa sifa
zitakazotumika kuwa ni ufaulu wa waombaji katika mitihani yao ya elimu
ya sekondari na diploma. Aidha, taarifa hizo zinaeleza kuwa maelezo
rasmi yanapatikana katika tovuti ya Bodi ya Mikopo na Tume ya Vyuo Vikuu
(TCU).
Bodi
inapenda kuwataarifu wadau wake wote, wakiwemo wale wanaotarajia kuomba
mikopo ya elimu ya juu kuwa taarifa hizo sio za kweli na kuwaomba wawe
na subira wakati Bodi inakamilisha taratibu za uombaji mikopo kwa mwaka
wa masomo 2016/2017.
Baada
ya kukamilika kwa taratibu hizo, mwongozo wa utoaji mikopo utatolewa
rasmi na kutangazwa kwa umma kupitia njia mbalimbali vikiwemo vyombo vya
habari na tovuti ya Bodi ya Mikopo www.heslb.go.tz
IMETOLEWA NA:
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU,
JUMANNE, JUNI 7, 2016
Taarifa hii pia inapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz)