Vijana, wadau na wanaharakati wamefungua vikundi
vya mtandao wa kijamii kwa ajili ya kuchanga fedha za
kumsaidia kijana wa Arusha aliyepatikana na hatia ya
kumtukana Rais na kuhumiwa faini ya Sh7 milioni au kifungo.
Kijana huyo, Isaack Habakuki wa Arusha alipatikana na hatia ya
kumtukana Rais kwa kutumia ukurasa wake wa facebook na
ametakiwa kulipa fedha hizo kwa awamu mbili na kuzikamilisha
ifikapo Julai 7 au kwenda jela miaka mitatu.
Diwani wa Kata ya Levolosi jijini Arusha (Chadema), Ephata
Nanyaro ambaye anaratibu michango hiyo kwa mkoa wa Arusha, alisema mpaka sasa
wameshakusanya Sh 800,000/ ambazo walizipata kwa njia ya kutuma kwa simu.
Alisema wanatarajia kupata Sh1.7 milioni kutoka mikoa yote.
"Tumesikia familia yake imeweza kutoa 3.5 millioni pekee, sisi tumejitolea kumsaidia ili afikishe 7 millioni kabla ya tarehe 7 mwezi julai,” alisema.