Mtu mmoja mkazi wa Kijiji cha Kandashi, wilayani Siha, mkoani Kilimanjaro, Abedi Akyo (53), amefariki dunia baada ya
kudaiwa kuchapwa viboko na wazee wa kimila kwa tuhuma ya
kujihusisha na wizi wa kuku.
Akielezea mazingira ya kifo hicho, Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro, Wilfred Mutafungwa amedai kuwa Akyo alichapwa
viboko 70 na wazee hao wa kimila wa Kimeru na Kimasai
Mutafungwa amesema watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya kuwasiliana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mwezi uliopita wakazi wa Kata ya Karansi wilayani hapa walitoa uamuzi kuwa wanawake
watakaovaa sketi fupi na vijana watakaovalia suruali chini ya kiuno, wataadhibiwa kwa kuchapwa
viboko 60 hadi 70.
