Watu 8 wamechinjwa na miili yao kutenganishwa na vichwa Jijini Tanga

Watu 8 wamechinjwa na miili yao kutenganishwa na vichwa akiwemo mjumbe wa serikali ya mtaa kufuatia vikundi vya uhalifu kuvamia nyumba za wakazi wa mtaa Kibatini uliopo kata ya Mzizima jijini Tanga hatua ambayo imeleta hofu kubwa kwa wananchi wa maeneo hayo.

Wakizungumza katika eneo la tukio baadhi ya waathirika ambao ndugu jamaa na zao wamechinjwa majira ya saa saba usiku wamesema kundi la watuhumiwa wanaokadiriwa kuwa walikuwa watu nane na kuvalia nguo nyeusi walipofika katika nyumba zao waliwaamuru akina baba watoke nje kisha kuwapeleka hadi katika vichaka kisha kuwachinja.
 
Tukio hilo limekuja wiki mbili tu baada ya vikundi hivyo vya uhalifu vinavyodaiwa kujificha katika mapango ya Amboni Mleni Maji moto kuchinja mbuzi 48,ng'ombe wawili na kuku zaidi ya 12 lakini Kamanda wa Polisi amekiri kuwa tukio hilo ni kubwa na kwamba jitihada za polisi zinafanywa ili kuhakikisha kuwa watuhumiwa wanakamatwa na kutiwa mbaroni. 
 
Hata hivyo ndugu wa mjumbe wa serikali ya mtaa wa Kibatini ambaye naye ni miongoni mwa waliochinjwa amesema chanzo cha kundi hilo kuwafanyia unyama huo inatokana na kukamatwa kwa watoto wa watuhumiwa ambao ndio waliokuwa wakitumwa kabla makundi hayo hayajafanya uhalifu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo