Wananchi wa Tandala Makete wakomalia suala la Maji, Huu ndio uamuzi wao (Audio)

Wananchi  wilayani Makete mkoani Njombe wameaswa kutunza miradi ya maji na kuiona ni miradi ya kwao ili kuondoa uhaba maji unaotokea katika maeneo yao pindi miradi hiyo inavyotumiwa vibaya.

Kauli hiyo imetolewa na msimamizi wa mradi wa maji wa kitongoji cha Kilovoko Bw, Naumu Tweve alipokuwa akizungumza na kituo cha Green Fm kwenye Chanzo cha maji cha Kilovoko Kilichopo kijiji cha Tandala kata ya Tandala wilayani hapa.

Bw. Naumu amewasisitiza wananchi kutunza vyanzo vya maji  na kuwa na fedha za akiba zitakazosaidia katika uboreshaji wa mradi huo na kufanya usafi katika chanzo hicho pale inapohitajika.

Wananchi waliokuwepo katika shughuli ya ukarabati wa mradi huo wamesema wameopokea vizuri huku wakilalamikia kitendo cha uongozi wa kijiji kushindwa kujitokeza katika zoezi hilo.

Bi Dora Chaula ni mwenyekiti wa kitongoji Cha Kilovoko naye akawashukuru wananchi kwa ushirikiano waliouonesha katika utekelezaji wa mradi huo.

Akijibu tuhuma za uongozi wa kijiji kutofika katika zoezi hilo Afisa mtendaji wa kijiji cha Tandala Bw Ambele Sanga amesema wakati zoezi hilo likiendelea yeye alikuwa kwenye majukumu mengine ya kikazi huku pia akisema mwenyekiti wa kijiji hicho alikuwa msibani ndiyo maana wameshindwa kufika.

Na Asukile Mwalwembe


 Wananchi wakiunganisha mabomba



 Msimamizi wa shughuli Bw. Nahom Tweve

 Chanzo cha maji
 Mwenyekiti wa kitongoji cha Kilovoko Bi Chaula akizungumza nasi

Wananchi wakiwa kazini


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo