Ishu ya wananchi kukosa vyoo yaibuka Ikonda Makete, Ni aibu (Audio)

Wananchi wa kitongoji cha ikonda bondeni kjiji cha ikonda kata ya tandala wilayani makete mkoani Njombe kwa pamoja wamekubaliana kuhakikisha kila kaya inakuwa safi ndani ya mwezi mmoja kuanzia leo.

Hayo yamezungumzwa na wananchi wa kitongoji hicho katika mkutano uliofanyika hii leo kutokana na kukithiri kwa uchafu katika maeneo yao huku baadhi ya kaya zikikosa vyoo pamoja na njia kutopitika kiurahisi kutokana na uchafu.

Wananchi hao wakizungumza mbele ya mwenyekiti wao wa kitongoji Bi Dora Mbilinyi na mwenyekiti wa kijiji Alexander Mbilinyi wamekubaliana kuimaliza kero hiyo ndani ya Mwezi mmoja.

Akichangia hoja katika mkutano huo mwenyekiti wa kijiji cha Ikonda Bw, Alexander Mbilinyi amesema suala la usafi ni nyeti hivyo linahitaji utekelezaji Wa haraka na kuitumia ipasavyo siku iliyopangwa na serikali ya kufanya usafi juma mosi ya kila mwisho wa mwezi.

Katika hatua nyingine wananchi hao wameongeza kuwa kutofanya usafi ni aibu kubwa hivyo wananchi wajifunze kufanya usafi katika kaya zao.
 mwenyekiti wa kijiji cha Ikonda Bw, Alexander Mbilinyi

 Wananchi wakisikiliza hoja


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo