Wananchi wilayani Makete mkoani Njombe wameaswa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuwabaini watu wanao wadhania kuwa ni wahalifu kwani itasaidia kuepusha vitendo vya kihalifu katika maeneo yao.
Hayo yamesemwa na baadhi ya wananchi waliofika katika kituo cha polisi Tandala Hii leo mara baada ya kuwafikisha watu wawili waliokuwa wanadhaniwa kuwa wezi kituoni hapo waliojulikana kwa majina ya James Mbilinyi na Elia Mbilinyi wakazi wa Wangama Njombe.
Katika kituo hicho cha polisi Tandala wananchi walikumbwa na taharuki na hali ilikuwa hivi.
Aidha kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Tandala Andowisye Memba akizungumza kituoni hapo amewapongeza wananchi kwa kutoa ushirikiano kwa watu wanao wadhania kuwa si watu wema.
Pia wananchi waliofika kituoni hapo Walioporidhishwa na maelezo kutoka kwa watuhumiwa baada ya kuhojiwa na jeshi la polisi, waliridhika na maelezo yao na kuliachia jeshi la polisi ili kukamilisha taratibu zinazofuata.
Na Asukile Mwalwembe
