Chiza Dastan (31), anayesadikiwa kuwa mwizi wa
pikipiki amefariki dunia Hospitali Wilaya ya Bukombe akipewa matibabu baada ya kupigwa na nyundo kichwani wakati
akijaribu kupora pikipiki.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo
alisema tukio hilo lilitokea Mei 20 saa 4.00 usiku nje ya Baa ya
Geen View, Kata ya Katente wilayani hapa.
Mwabulambo alisema Chiza ambaye ni mkazi wa Kilimahewa, alifariki dunia wakati akitibiwa
baada ya kujaribu kupora pikipiki ya Nassoro Tadeo aliyemkodi kutoka mjini Ushirombo kwenda
kwenye baa hiyo.
Alisema wakiwa nje ya baa, ghafla mhalifu alianza kuongea na watu
wasiojulikana kwenye simu, mwendesha bodaboda alishtuka na kutaka kuondoka.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya, Dk Mahona Kaji alisema majeruhi alipokelewa akiwa na hali mbaya kutokana na kupondwa na kitu kizito kichwani, fuvu la kichwa lilionekana limepasuka.
Dk
Kaji alisema walijitahidi kuokoa maisha yake lakini ikashindikana.